Akiongea na wanachi mjini Bukoba naibu wa waziri wa elimu tamisemi
kasim majaliwa ambae alikuwa mgeni rasimi katika harambee ya kuchangisha
pesa zitakazo tumika katika ujenzi wa maabara amesema zoezi la ujenzi
wa maabara katika shule za sekondari si la wananchi pekee ambapo
ameongeza kuwa serikali imetenga bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni
moja ambazo zitatumika kununua vifaa vya maabara zote zinazojengwa
nchini nakwamba zoezi la ujenzi wa maabara limekuwa likikabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wafedha ambapo amewataka wadau wa
elimu na taasisi mbalimbali zenye uzalendo na taifa hili basi wajitokeze
ili kuchangia ujenzi wa maabara kwaajili ya kukuza kiwango cha elimu
hapa nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya
Bukoba Adoh Mapunda amesema wananchi wa manispaa ya Bukoba wamejitahidi
kwa kiasi kikubwa katika kuchangia michango mbalimbali kwaajili ya
ujenzi huo lakini pamoja na michango ya wananchi halimashauri ya
manispaa hiyo imelazimika kufanya halambee hiyo kwaajili ya kuchangisha
fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa elimu kwalengo la kukamilisha
zoezi hilo la ujenzi wa maabara kwaajili ya kutekeleza agizo la rais wa
jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Nao baadhi ya wadu mbalimbali waelimu waliojitokeza katika harambee
hiyo wamezitaka halmashauri nyingine nchini kuiga na kufuata mfano
uliotumiwa na halmashauri ya manispaa ya Bukoba kwa kuanzisha harambee
ambayo imefanikisha kupatikana kwa pesa tasilimi zaidi shilingi miloni
arobaini na nne hali ambayo sasa inaleta matumaini ya kukamilisha ujenzi
wa maabara katika shule zote za sekondarai zilizopo katika manispaa
hiyo.
Post a Comment