0

KITAMBI: ALIIPANDISHA NDANDA FC, IKAANZA NA USHINDI LIGI KUU IKIWA UGENINI SHINYANGA.
Ndanda FC imemfuta kazi kocha wake, Denis Kitambi.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa ndanda zinaeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo umechukua uamuzi huo baada ya vipigo viwili dhidi ya Mtibwa Sugar na kile cha nyumbani jana dhidi ya Ruvu Shooting.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Kocha wa Makipa, Mohammed Mwarami 'Shilton' naye ametimuliwa pia.
Imeelezwa kumekuwa na kikao cha dharura  na viongozi wamefikia uamuzi huo.
Juhudi za kuwapata viongozi wa Ndanda FC zimekuwa zikikwama kutokana na viongozi hao kutopokea simu.
Lakini mchezaji mmoja wa Ndanda FC amelithibitisha hilo.
“Tumeambiwa kuwa wamemtimua kocha, ila bado viongozi hawajafika kutueleza,” alisema.

Post a Comment

 
Top