0

Lee Joon-seok (Aliyefungwa pingu)aliyekuwa nahodha wa Mv Sewol akifikishwa mahakamani.
Upande wa mashtaka wa kesi inayowakabili nahodha Lee Joon-seok (68) na wenzake 11 waliokuwa wafanyakazi katika meli iliyozama mwezi Machi mwaka huu Korea Kusini wameitaka mahakama ya nchi hiyo kutoa hukumu ya kifo kwa washtakiwa hao kutokana na kesi inayowakabili ya kusababisha mauaji ya binadamu yaliyotokana na uzembe.
Wakielezea kuhusiana na hukumu hiyo, upande wa mashtaka umesema washtakiwa hao wanastahili adhabu hiyo kutokana na kitendo cha kutofanya jitihada zozote za kuwaokoa abiria waliokuwemo katika meli hiyo, na badala yake wakajiokoa peke yao.
Ajali hiyo ilitokea Aprili 16 mwaka huu, ambapo meli hiyo Mv Sewol ilipata ajali ikiwa na abiria zaidi ya 470, ambapo kati yao zaidi ya watu 300 walifariki wengi wao wakiwa ni wanafunzi.
Hukumu ambayo imependekezwa na upande wa mashtaka umeitaka mahakama hiyo kumhukumu Joon-seok hukumu ya kifo, na wasaidizi wake 3 hukumu ya kifungo kati ya miaka 15-30.
Nahodha wa meli hiyo amejitetea kuwa wakati ajali hiyo ikitokea alichanganyikiwa na kushindwa kufanya maamuzi juu ya namna ya kuwaokoa abiria waliokuwemo ndani ya meli hiyo.

Post a Comment

 
Top