Mashuhuda wakieleza yaliyotokea.
LORI la
mafuta aina ya Scania likiwa limesheheni dizeli likitokea bandarini
jijini Dar es Salaam kuelekea mikoani, liligonga tuta katika Barabara ya
Morogoro, eneo la Kimara-Baruti, likapoteza mwelekeo na kupinduka
kisha kuwaka moto na kuteketea kabisa.
Wakati
lori hilo likiwaka, mafuta yenye moto yalisambaa na kutaka kuunguza
nyumba za jirani lakini Kikosi cha Uokoaji na Zima Moto cha Halmashauri
ya Jiji, kiliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo.
Tukio hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa magari yanayotumia njia hiyo kutokana na sehemu hiyo kupitika kwa shida.
(HABARI/PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )
Post a Comment