Shirika
la afya ulimwenguni WHO limesema dawa ya Ebola ambayo imetengenezwa kwa
mchanganyiko na damu ya watu waliambukizwa na kisha kupona ugonjwa wa
Ebola inatarajiwa kuanza kupatikana wiki chache zijazo huko Afrika
Magharibi.
Afisa
mwandamizi wa W.H.O. Dr Marie Paule Kieny amesema vifaa vimetolewa
Liberia kwaajili ya kupata damu na vifaa vya kufanyia utafiti huo wa
dawa ili kupata dawa Serum.
Dr Kieny akizungumza mjini Geneva amesema kuwa kazi ya mapambano dhidi ya Ebola harakati za upatikanaji chanjo ya ugonjwa huo .
Maelfu ya watu wanatarajiwa kutumiwa katika majaribio hayo yanayolenga kupatikana kwa chanjo na dawa ya ugonjwa huo
Post a Comment