Kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, ameongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo akisaini miaka miwili.
Awali,
kiungo huyo mwenye kasi kubwa uwanjani, alisaini mkataba wa miezi sita
ya kuichezea timu hiyo akitokea Yanga, akiondoka kwa mgogoro mkubwa.
Meneja wa
kiungo huyo, Abdulfatah Saleh,alisema kuwa Okwi ameongeza mkataba huo
baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili kati yao na klabu hiyo.Abdulfatah
alisema, awali kiungo huyo alisaini mkataba mfupi wa kuichezea Simba
ili kupisha kesi iliyopo kati yake (Okwi) na Yangailiyomfungulia
mashtaka kwa madai ya kukiuka makubaliano yaliyokuwepo kwenye mkataba.
Aliongeza
kuwa, mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo iliyosimamiwa na Kamati
yaSheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), ndiyo akaongeza mkataba huo mwingine.
“Okwi
ameongeza mkataba mwingine wa kuichezea Simba, amesaini mkataba wa miaka
miwili baada ya kesi yake na Yanga kumalizika kwa TFF kumruhusu
kuichezea Simba kufuatia timu ya zamani kushindwa kutimiza makubaliano
yaliyokuwepo kwenye mkataba wake.
“Mwanzoni
alisaini mkataba wa miezi sita ili kupisha kesi hiyo imalizike, awali
alisaini mkataba huo kwa hofu ya kushindwa kesi hiyodhidi
ya Yanga,” alisema Abdulfatah.
Post a Comment