Na Baraka Mpenja, Dar Es salaam
MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans wameibuka
na ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa
ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa jioni hii uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam.
Yanga
walikuwa wa kwanza kuliona lango la Kagera Sugar katika dakika ya 3 ya
kipindi cha kwanza kupitia kwa Mganda Hamis Kiiza `Diego` kufuatia
kumalizia krosi nzuri iliyochongwa na winga machachari, Mrisho Khalfan
Ngasa.
Yanga waliandika bao la pili katika dakika ya 34 kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Burundi, Didier Kavumbagu.
Kagera
Sugar walifunga bao la kufutia machozi katika dakika ya 63 kupitia kwa
Daudi Jumanne baada ya beki wa pembeni wa Yanga, Oscar Joshua kuzembea
kuosha mpira katika eneo lao la hatari.
Kwa
matokeo hayo, Yanga wanafikisha pointi 52 baada ya kucheza mechi 24,
pointi moja nyuma ya vinara Azam fc walioshindwa kucheza mechi yao ya 24
leo hii dhidi ya Ruvu Shooting baada ya mvua kubwa kunyesha na uwanja
wa Mabatini mkoani Pwani kuwa katika hali mbaya.
Mchezo
wa leo ulikuwa muhimu kwa Yanga, hivyo wamepambana nadani ya dakika
zote 90 kutafuta ushindi, ingawa Kagera Sugar walionekana kuwa imara kwa
kiasi kikubwa.
Kosakosa
kwa timu zote zimeshuhudiwa ndani ya uwanja wa Taifa, na dakika za lala
salama Kagera walikuwa wanawashambulia Yanga kutafuta bao la pili la
kusawazisha, lakini mabeki walikuwa makini kuzuia hatari hizo.
Hata
hivyo, yanga wangepata mabao mengi zaidi kama isingekuwa uzembe wa
washambuliaji wake, Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa na
Hussein Javu.
Kwa
nyakati tofauti, washambuliaji hawa walipata nafasi za kufunga, lakini
walipungukiwa maarifa ya kumtungua kipa wa Kagera Sugar, Agaton Antony.
Sasa
Yanga wamebakiza mechi mbili dhidi ya JKT Oljoro mwishoni mwa wiki hii
katika uwanja wa Shk. Amri Abeid jijini Arusha, na watafunga msimu na
Simba aprili 19 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Hali ya uwanja wa Mabatini ilikuwa namna hii leo
Ili
kutetea ubingwa wao, Yanga wanatakiwa kushinda mechi zote mbili, huku
wakiwaombea dua mbaya Azam fc wenye michezo mitatu mkononi.
Endapo
Yanga watashinda mechi zao mbili walizobakiza, watafikisha pointi 58
ambazo Azam fc wataweza kuzivuka kama watashinda mechi mbili tu kati ya
tatu walizosaliwa nazo.
Nafasi ya ubingwa bado ni wazi na mpaka sasa huwezi kutabiri nani atatwaa ndoo msimu huu.
Mechi
nyingine ilitakiwa kupigwa katika dimba la Mabatini, Mlandizi mkoani
Pwani baina ya wenyeji wa uwanja huo, Maafande wa Ruvu Shooting dhidi ya
Vinara Azam fc, lakini mechi hiyo imeahirishwa mpaka kesho baada ya
mvua kubwa kunyesha na kuharibu mandhari ya uwanja huo na sasa mechi
hiyo atachezwa hapo kesho.
Licha ya Yanga kushinda leo, Azam fc bado wapo kileleni kwa pointi moja zaidi ya Yanga, lakini wana michezo mitatu mkononi.
Kama
watashinda mchezo wao wa 24 hapo kesho, basi watakuwa wanahitaji pointi
tatu tu katika mechi mbili zitakazobaki ili kujitangazia ubingwa msimu
huu.
Mechi
ya kesho itakuwa na ushindani mkubwa kwa Azam fc kutokana na rekodi ya
Ruvu Shooting katika dimba la Mabatini ambapo wanaonekana kuwa wagumu na
hutoa ushindani mkubwa zaidi.
Baada
ya mechi ya kesho, Azam fc mwishoni mwa wiki watasafiri kwenda Mbeya
kuwafuata wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City katika dimba la Sokoine
jijini humo.
Hii
itakuwa mechi ngumu zaidi kwa kocha Joseph Marius Omog wa Azam fc
kwasababu Mbeya City wapo katika ushindani wa nafasi ya pili msimu huu.
Pia hawana rekodi ya kufungwa katika dimba lao tangu kuanza kwa msimu huu.
Si Yanga wala Simba aliyetoka na pointi tatu katika uwanja huo mgumu kwa timu vigogo.
Baada ya Mbeya, mechi ya mwisho kwa Azam fc itakuwa aprili 19 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, aprili 19 mwaka huu
Post a Comment