0

Dawa ya Tamiflu
Wanasayansi nchini Uingereza wamesema serikali duniani zinapoteza mabilioni ya fedha kwa kuhifadhi dawa za tibu homa ya mafua makali, dawa ambayo matokeo yake yanatiliwa mashaka.
Serikali mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza zilihifadhi dawa ya Tamiflu katika bohari zao, huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea mlipuko wa mafua ya ndege.
Watafiti kutoka kampuni ya dawa ya Cochrane Collaboration na jarida la masuala ya utabibu la British Medical Journal, wamesema hakuna ushahidi mzuri unaobainisha kuwa dawa ya Tamiflu imepunguza idadi ya watu wanaougua na kulazwa hospitali au madhara yanayosabishwa na virusi vya mafua.
Wamesema kama kuna faida ya dawa hizo basi ni ndogo lakini kuongeza hatari ya mafua.
Hata hivyo kampuni inayozalisha dawa hizo, Roche na watalaam wengine wamesema uchambuzi huo una dosari, huku wakisema kimsingi haikubaliani na utafiti huo.
Uingereza imetumia pauni £473m kununulia dawa ya Tamiflu, ambayo imejazana katika bohari za dawa duniani kote kujiandaa kwa mlipuko wa mafua makali.
Jopo la wataalam waliotoa ripoti ya dawa ya Tamiflu
Dawa hiyo ya Tamiflu imekuwa ikihifadhiwa nchini Uingereza tangu mwaka 2006 wakati baadhi ya mashirika yalikuwa yakitabiri kuwa ugonjwa wa mafua ya ndege ungeweza kuua watu wapatao 750,000 nchini Uingereza. Uamuzi kama huo ulifanyika katika nchi nyingine duniani.
Dawa hiyo ilishauriwa kwa kiasi kikubwa itumike wakati wa mlipuko wa mafua ya nguruwe mwaka 2009.
Kampuni za dawa hazichapishi taarifa zao zote za utafiti. Ripoti hii ni matokeo ya mvutano kuhusu taarifa iliyofichwa zamani kuhusu ufanisi na madhara ya dawa aina ya Tamiflu.
Ripoti hiyo imehitimisha kuwa dawa hiyo ilipunguza dalili za homa ya mafua kutoka siku saba hadi siku 6.3 kwa wakubwa na kwa watoto siku 5.8.Taarifa ya wahariri wa ripoti hiyo wanasema dawa kama paracetamol zingeweza kuwa na ufanisi sawa na hiyo.
Kuhusu madai kwamba dawa hiyo ilizuia madhara ya pneumonia, Cochrane wanasema majaribio hayo yalikuwa dhaifu sana kiasi kwamba "hakuna matokeo mazuri yaliyobainika".
Carl Heneghan, Profesa wa Evidence-Based Medicine katika chuo kikuu cha Oxford na mmoja wa wahariri wa ripoti hiyo ameiambia BBC: "Nafikiri fedha yote £500m haijanufaisha afya ya binadamu na huenda tumewadhuru watu kutokana matumizi ya dawa hizi.

Post a Comment

 
Top