Watu 11 wamepoteza maisha papo hapo na mwingine mmoja kufariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.
Basi hilo
liligonga nyumba kisha kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi
katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Yitwimila kata ya
Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Mbali na
watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa
chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi wa sasi hilo ambapo dereva wa
alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga
nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na
Akizungumza
na waandishi wa habari katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika
ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7.
Walioshuhudia
ajali hiyo wamesema kabla ya kutokea kwa ajali hiyo basi hilo lilianza
kuyumba na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara
hiyo.
Mganga
mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe
alithibitisha kupokea majeruhi 60 pamoja na maiti 11.
Amesema
kati ya majeruhi hao 25 hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika
hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi
waliobaki katika hospitali hiyo zinaendelea vizuri na tayari wengine
wameanza kuruhusiwa.
Jeshi la polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
>>>>via dunia kiganjani
Post a Comment