Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewataka viongozi nchini kuacha kuwatumia wananchi kama chambo cha
kufanikisha malengo yao ya kisiasa na kusababisha migororo na uvunjifu
wa amani.
Aidha,
Rais Kikwete amewataka wananchi wa Wilaya ya Karatu wasiige mfano wa
Arusha ambako fujo zinazoongozwa na baadhi ya viongozi zimezorotesha
sana uchumi wa mji huo kwa sababu usalama ni kigezo kikuu cha maendeleo
ya uchumi.
Akizungumza wakati anazindua Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, mjini Karatu asubuhi ya leo, Jumanne, Aprili 22, 2014, Rais Kikwete amesema:
“Usalama
ni jambo muhimu sana na kwa maana hiyo, nawaombeni msiige kabisa mfano
wa Arusha, sote tunajua kimetokea nini kule kwa sababu ya fujo za
kisiasa ambazo zinachochewa na viongozi na hasa Mbunge wa Arusha mjini
Bwana Lema,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mbunge
anayo nafasi kubwa kujenga hoja zake ndani ya Bunge na ndani ya
mikutano ya halmashauri. Lakini kwa mbunge kuwachochea wananchi na
kuwachukua na kuwatembeza barabarani ambako wanakumbana na virugu vya
polisi siyo uongozi wa busara hata kidogo.”
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mheshimiwa Lazaro Titus
Massey amewaambia wananchi kuwa moja ya mwelekeo mkuu wa CHADEMA
wilayani Karatu ni kushirikiana na Serikali na polisi katika kudumisha
amani.
Tunawakaribisha
Arusha waje kujifunza kwetu namna ya kudumisha amani. Tunamkaribisha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Bwana John Mongella kuja kujifunza namna
ya kurejesha na kudumisha amani mjini humo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
22 Aprili,2014
Post a Comment