0
MATUKIO YA KISIASA
Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen


Umoja wa Kujihami-NATO umesimamisha ushirikiano wake na Urusi kufuatia mgogoro wa Crimea na kuhoji madai ya taifa hilo ya kuondoa majeshi yake karibu na mpaka wa Ukraine kwa kusema bado kuna utata. 

Bunge la Marekani jana lilipitisha fungu kwa ajili msaada kwa Ukraine sambamba na vikwazo dhidi ya Urusi kufuatia kitendo chake cha kulichukua eneo la Crimea. 

Shinikizo la hivi karibuni la mataifa ya Magharibi dhidi ya Urusi linatolewa wakati uchumi wa Ukraine ukiyumbayumba na bei ya bei gesi ikizidi kuongezeka. Hiyo inatajwa kuwa ishara mbaya zaidi baina ya pande mbili za Mashariki na Magharibi tangu kumalizika Vita Baridi.

Bunge la Ukraine litakuwa imefikia moja ya malengo kwa kupiga kuyapokonya silaha makundi yanayojihami kwa silaha yaliyoibuka katika maeneo tofauti ya taifa hilo katika kipindi cha vurugu za kisiasa, ambazo kwa mara ya mwanzo zilizuka mwishoni mwa Novemba mwaka uliyopita kufuatia uamuzi wa serikali ya zamani ya taifa hilo kukataa makubaliano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya.

Lengo na ushirikiano na NATO

Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO

Serikali ya mjini Kiev, imesema kujiunga na NATO haikuwa kipaumbele chao katika lakini pia inaweza kuwaongezea uwezo wa kukabili vishindo vya Urusi. 


Lakini mvutano umeendelea kuwa katika kiwango cha juu kabisa kwa zaidi ya wiki mbili sasa baada ya Urusi kulichukua eneo la Crimea na katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen akisema umoja huo umesimamisha ushirikiano wote wa kivitendo na Urusi, kijeshi na kiraia.

Hata hivyo amesema ile fursa ya kidiplomasia kwa taifa hilo bado wameiwacha wazi. Aidha aliongeza kusema hawezi kuthibitisha kama Urusi imeondoa majeshi yake karibu na mpaka Ukriane. Akizungumza wakati mawaziri wa mambo ya nje wakikutana kwa siku mbili mjini Brussels, Rasmussen amesema "hicho sicho walichokiona"

Kufuatia msimamo huo wa NATO wa kusimmisha ushirikiano wake na Urusi. Serikali ya taifa hilo imeuhtuhumu umoja huo kwa kusema inarejesha lugha ya Vita Baridi ili isimamishe ushirikiano wao. Na kuongeza kuwa hakuna upande wowote utakaonufaika na hatua hiyo.

Urusi imejiandaa vyema kijeshi Taarifa nyingine kutoka mjini Brussels zianeleza Kamanda wa juu wa jeshi wa NATO Jenerali Philip Breedlove amesema Urusi umejitosheleza kijeshi katika mpaka wa taifa lake na Ukraine na endapo itataka kutekeleza matawa yake basi jambo hilo linawezekana katika kipindi cha siku tatu hadi tano. Anasema amebaini harakati za jeshi hilo jana usiku lakini hakuna dalili kama wanarejea makambini.

Ukraine na Marekani zimekuwa zikihituhumu Urusin kwa kukusanya maelfu ya wanajeshi wake karibu na mpaka na kuonesha wasiwasi wao kwamba uenda zikataka kulichukue eneo la kusini la Ukraine, eneo ambalo wakazi wake wengi wenye asili ya Kirusi.DW
 

Post a Comment

 
Top