Morocco imetangaza kuwa
inakifyeka kile ilichoeleza kuwa kikundi kipya cha magaidi ambacho
kinaajiri watu wa kwenda kupigana Syria.
Katika taarifa yao, polisi wa Morocco walisema
kuwa kikundi hicho kilishirikiana na waakilishi wa mashirika yaenye
uhusiano na al-Qaeda kama "taifa la Kiislamu la Iraq na Mashariki ya
Mediterranean", ISIS, na kundi la al-Nusra Front.Polisi walisema kikundi hicho cha Morocco kiliwapatia mafunzi vijana kabla ya kuwatuma kupigana nchini Syria, na kwamba kinakusanya fedha kugharimia safari hizo za kuwapeleka Syria.
Mkuu wa mashtaka wa Morocco ameanzisha uchunguzi.BBCSWAHILI
Post a Comment