Magazeti
mjini Nairobi yalibeba vichwa vya habari siku ya Jumatano (tarehe 2
Aprili) kutoa taarifa juu ya kifo cha mhubiri wa Kiislamu Sheikh
Abubakar Shariff Ahmed, anayejulikana kama Makaburi, ambaye alipigwa
risasi Jumanne
Kama habari zivyotoka Jumanne usiku (tarehe 1 Aprili) kwamba watu wenye silaha wasiojulikana walimuuwa Mhubiri wa Kiislamu wa Kenya Sheikh Abubakar Shariff Ahmed, anayejulikana kama Makaburi, Mamlaka za Mombasa zilitarajia maandamano ya vurugu sawa na yale yaliyoshuhudiwa baada ya wakuu wa dini awali kupigwa risasi kwa njia kama hiyo.
"Makaburi
na mtu wa pili aliyejulikana kama Hassidh Bahero waliigwa risasi na
watu wasiojulikana nje ya Mahakama za Shanzu," mkuu wa Idara ya
Uchunguzi wa Jinai wa Kaunti ya Mombasa Henry Ondiek aliiambia Sabahi.
"Watu wengine watatu walinusurika na mauaji hayo ya kufyatua risasi
kutoka kwa gari linalopita."
"Hata na sisi tunashangazwa na mauaji haya lakini tumeanza uchunguzi mara moja ili kuwatambua wauaji na sababu zao," alisema.
Ondiek
alipuuza madai ya baadhi ya wananchi wa Kenya na viongozi kwamba polisi
wanaweza kuwa walimuua Makaburi kutokana na msimamo wake mkali na
mahusiano yake na al-Shabaab.
Mwili wa
Sheikh Abubakar Shariff Ahmed "Makaburi" unateremshwa kutoka gari la
polisi Jumanne usiku. Mhubiri huyo alizikwa takriban saa sita usiku na
kusifiwa na wafuasi wake kama "shahidi".
"Ni
kawaida kwamba polisi kuwa ni washukiwa wa kwanza kwa sababu
tunatafuatia ugaidi na mashtaka yanayaohusiana na uchochezi na ghasia
dhidi yake," Ondiek alisema. "Lakini tulikwishaliachia hilo kwa mahakama
za sheria. Mbali na hilo, yeye aliheshimu amri za mahakama na alikuwa
akiripoti polisi kila Jumanne ."
Makaburi
alikuwa kiongozi matata aliyehusishwa na Masjid Mussa mjini Mombasa,
ambao uliitwa jina jipya la Masjid Shuhadaa mwezi uliopita, na ulikuwa
katika orodha za kimataifa za vikwazo kwa kuuunga mkono vikundi vya
kigaidi.
Alhamisi
iliyopita tu (tarehe 27 Machi ), mahakama ya Mombasa ilimzawadia
Makaburi shilingi 670,000 (dola 7,700) katika fidia na madhara maalumu
baada ya Mahakama Kuu kuamua kuwa uvamizi wa polisi kwa nyumba yake
ulikiuka haki zake za kikatiba.
Abubakar
Shariff Ahmed, anayejulikana kama Makaburi, wakati alipofikishwa
mahakamani mjini Mombasa tarehe 6 Septemba, 2012. [Na Bosire
Boniface/Sabahi]
Mkurugenzi
wa Mashitaka ya Umma Keriako Tobiko pia aliripotiwa kuwa katika
mchakato wa kuomba kuhamishwa kwa kesi ya Makaburi kupelekwa katika Jela
ya Shimo la Tewa kwa sababu za kiusalama.
Makaburi
na wenzake waliripotiwa kuwa walikuwa wanasubiri matatu nje ya Mahakama
za Sheria za Shanzu, ambako walitakiwa kutipoti kila wiki, wakati
walipofyatuliwa risasi.
Waandamanaji wa amani watoa wito wa haki
Shuhuda
Abdulahi Jama Abdi, mwenye umri wa miaka 29, mkazi wa Mombasa, alisema
kwamba upigaji risasi huo ulianza dakika chache kabla ya saa 1 jioni.
"Ilikuwa
ni jioni, lakini mtu anaweza kuona wazi gari ndodo nyeupe inakaribia
eneo la tukio na kukimbia mara baada ya milio ya risasi," aliiambia
Sabahi. "Ilikuwa ni baadaye sana ndipo tulipojuwa kuwa ni Makaburi
ambaye alipigwa risasi. Watu wawili [wanaume] waliweka mwili wa marehemu
umbali wa mita moja katika dimbwi la damu juu ya migongo yao juu ya
barabara ya pembeni."
Abdi
alisema kundi la watu walifanya maandamano ya amani katika eneo la tukio
wakati wa usiku, na kuongeza kwamba walikuwa wamekasirishwa na mauaji
yasiyoelezwa ya ulamaa wa Kiislamu wenye msimamo mkali huko Mombasa.
Alisema waandamanaji walituhumu polisi kuhusika na mauaji hayo.
Kifo cha
Makaburi kinakuja baada ya ulamaa wa Kiislamu Aboud Rogo Mohammed,
ambaye pia alikuwa katika orodha za kimataifa za vikwazo kwa kuiunga
mkono al-Shabaab, aliuliwa mwezi wa Agosti 2012 katika mauaji kama hayo
ya kupigwa risasi kutoka kwenye gari.
Mrithi wa
Rogo Sheikh Ibrahim Ismail na watu watatu wengine waliuawa katika kwa
kupigwa risasi kutoka garini mwezi Oktoba 2013, na kuzua machafuko mjini
Mombasa yaliyosabaisha kifo cha angalau mtu mmoja na wengine kadhaa
kujeruhiwa.
Katika kesi zote mbili, polisi hawajawatia mbaroni washukiwa wowote na vifo hivyo vimepita bila ya kuadhibiwa mtu yeyote.
Duale: Mauaji kinyume na sheria hayatashinda vita vya ugaidi
Kiongozi
wa Wengi katika Bunge la Taifa la Kenya na mbunge wa Mji wa Garissa Aden
Duale alisema kwamba polisi wanapaswa kufanya haraka kuchunguza mauaji
hayo.
"Kama ni
mauaji kinyume na sheria, yanaweka historia mbaya kwamba hawezi kushinda
vita dhidi ya ugaidi nchini Kenya, "aliiambia Sabahi." Mauaji haya ya
karibuni ynaweza kutazamwa kama ni pigo kubwa kwa siasa kali nchini
Kenya, lakini kwa upande mwingine yanawafanya baadhi ya vijana kuwa sugu
ambao wanaweza [kufikiri] kwamba serikali inalenga imani moja katika
vita dhidi ya ugaidi. "
Duale
alisema uungaji mkono wa Makaburi wa al-Shabaab na kuhalalaisha kwake
shambulio la Jumba la Maduka ya Biashara la Westgate mjini Nairobi --
ambayo Makaburi alielezea kama "halali kwa asilimia 100" --kulimtenga na
wahubiri wenye siasa kali.
"Wakuu wa
dini wachache wana ujasiri kama huo wa kuwa wazi na kuviunga mkono
vikundi vya kigaidi, lakini licha ya hiyo, hakuna haki kwa polisi kumuua
[wakati] tumefanyia marekebisho mahakama kusimamia haki," alisema.
Duale aliomba utulivu miongoni mwa jamii ya Waislamu ili kuruhusu uchunguzi.
Wasiwasi watanda Mombasa, Nairobi lakini tulivu
Kama
ilivyokuwa kwa vifo vya Rogo na Ismail, kifo cha Makaburi pia kimeleta
wasiwasi Mombasa ambapo maulamaa hao walikuwa waungaji mkono wengi, na
Mkuu wa polisi wa Kaunti ya Mombasa Robert Kitur aliiambia Sabahi kwamba
wako katika uangalizi wa machafuko.
"Limekuwa
tukio la bahati mbaya kwamba wafanya fujo wachache watataka kulitumia
tukio hili, lakini vikosi vya usalama viko katika tahadhari kubwa kuzuia
machafuko, uharibifu wa mali na upotevu wa maisha," alisema, akiongezea
kwamba watachukua tahadhari hususani Ijumaa wakati wa swala na
kuzunguka msikiti wa Shuhadaa.
Polisi
waliojihami walikipiga doria katika mitaa ya Mombasa Jumatano baada ya
Makaburi kuzikwa muda mfupi baada ya saa sita usiku na kusifiwa na
wanaomuunga mkono kama shahidi.
Wito wa
utulivu kutoka kwa maulama wa Kiislamu kupitia vipaza sauti kwenye
msikiti wa Shuhadaa uliendelea usiku wote, AFP iliripoti, na miito kama
hiyo ilitolewa kupitia vituo vya redio za ndani.
Lakini
ingawa kulikuwepo hali ya wasiwasi na polisi na vikosi vya ulinzi vikiwa
vimesambazwa kwa wingi -- ikijumuisha walinzi wenye silaha kuzunguka
makanisa makuu katika maeneo yaliyo mahali pabaya -- Mombasa ilikuwa na
utulivu.
"Tunalaumu
mauaji ya kutumia nguvu kubwa na tuko mbali na furaha hatika hali ya
usalama hapa ... mauaji haya yanapaswa kukoma," alisema Sheikh Muhdhar
Khitamy, mwenyekiti wa mkoa wa Baraza Kuu la Waislamu la Kenya.
"Hata hivyo, tunaomba utulivu kwa watu kutoonyesha hisia kwa vurugu," alisema.
Mitaa ya
Nairobi pia ilikuwa na utulivu pamoja na ongezeko la kuwepo kwa polisi,
ingawa habari za kifo cha Makaburi zilikuwa akilini mwa wengi Jumatano
asubuhi.
Wakili wa
haki za binadamu wa Kenya Mbugua Mureithi, ambaye alikuwa mmoja wa
wakili wa Makaburi, alilaani mauaji ya mteja wake na kutoa lawama moja
kwa moja kwa vikosi vya usalama vya Kenya.
"Nilipozungumza
na Makaburi, hakukiri kuwa na maadui wowote licha ya idara za usalama
ambazo alisema wakati wote zilikuwa zinamuandama," Mureithi aliiambia
Sabahi. Aliitaja mauaji ya Makaburi kuwa mauaji yasiyofuata sheria za
mahakama iliyofanya na vikosi vya usalama, mauaji ambayo yalikuwa ni
hatari yanayoweza kusababisha kutofaulu kwa vita dhidi ya ugaidi kwa
sababu yanaweza kusababisha kuwaingiza katika siasa kali vijana Waislamu
zaidi nchini Kenya.
"Mauaji
ni mbinu ya kizamani ambayo haina nafasi katika Kenya ya kisasa,"
alisema. "Hebu serikali iwe na ubunifu zaidi katika kushughulikia
changamoto za usalama zinazojitokeza."
Raia wa Nairobi wahofia kuenea kwa vurugu
"[Makaburi]
amekuwa akishawishi vita vya kidini kati ya Wakristo na Waislamu,
lakini bado, alikuwa ni mtu asiye na hatia hadi ingethibitishwa kuwa ana
hatia na mahakama," alisema Ken Mbugua, msaidizi wa mchungaji wa Kanisa
la Emmanuel Baptist huko Nairobi.
Mbugua
alisema itakuwa ni hali ya kusikitisha kama nchi itajipata yenyewe
ikitatua kutokubaliana kupitia vurugu badala ya mahakama.
"Hii
itazalisha machafuko na kuiingiza nchi katika matatizo makubwa
yanayofanana na ugomvi wa kidini uliotokea nchini Nigeria na Jamhuri ya
Afrika ya Kati," aliiambia Sabahi.
Kwa Mercy
Mumo mwenye umri wa miaka 25, keshia wa Duka kubwa la Nakumatt huko
Nairobi aliyepoteza rafiki yake wa karibu katika shambulio la maduka
makuu ya Westgate mwezi Septemba, kifo cha Makaburi kimeleta mwisho.
"Aliposema
mauaji yale ya kutisha ni halali pamoja na mauaji ya Wakristo na
uchomaji wa makanisa, nilijua alikuwa maiti inayotembea," aliiambia
Sabahi. "Ninaamini tutasahau kuhusu ukurasa huu wa huzuni na kuanzisha
Kenya yenye mshikamano zaidi."
Ibrahim
Hussein, mwenye umri wa miaka 27 anayeuza viatu karibu na Msikiti wa
Jamia huko Nairobi, aliwaomba waislamu kujizuia kuwafanyia vurugu
wasiokuwa waislamu wasiokuwa na hatia, kurudia kile kilichotokea wakati
Rogo alipouawa miaka miwili iliyopita.
"[Makaburi]
alikuwa muhubiri mchochezi na sikukubaliana na mafundisho yake,"
alisema. "Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa mauaji yake nje ya mahakama
ni halali. Ninatumaini Wakristo na Waislamu watashirikiana kwa amani
huko Mombasa na maeneo mengine ya nchi."
Chanzo: sabahionline.com
Post a Comment