jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius
Nyerere wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo, Kipawa. Rais Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe Jaap Frederiks baada ya kuweka
jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius
Nyerere wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo. Rais Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo.
Rais Kikwete akieleza jambo baada ya kupata maelezo ya ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo.
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kuanza ujenzi wa jengo la tatu la la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba , Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Injinia Suleiman Suleiman, na Mwenyekiti wa Kamatim ya Bunge ya Uchukuzi Mhe. Peter Serukamba.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameiamuru
Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake kuchukua hatua za mara moja kukomesha aibu
ya viwanja vya ndege vya Tanzania kutumika katika uchochoro wa kupitisha na
kusafirisha madawa ya kulevya.
Aidha,
Rais Kikwete amesema ukweli kuwa madawa ya kulevya yanazidi kupita katika
viwanja vya ndege za Julius Nyerere International Airport (JNIA) na ule wa
Kilimanjaro International Airport (KIA) unazidi kuchafua heshima na jina la
Tanzania.
Rais
Kikwete alikuwa anazungumza leo, Alhamisi, Aprili 24, 2014, kabla ya kuweka
jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius
Nyerere wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo.
Rais
ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Uwanja huo muda mfupi baada ya kuweka
jiwe la msingi kwenye Ujenzi wa Hospitali ya Kisasa ya Kufundishia na Kutoa
Huduma katika eneo la Mlongazila, eneo la Kibamba, Dar Es Salaam. Shughuli zote
mbili ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano.
“Siridhishwi
na hali ya usalama katika viwanja hivi viwili na matukio ya kusikia madawa
yametokea Tanzania kupitia viwanja vyake na yamekamatwa huko Australia
yanachafua sana jina la nchi yetu. Badala ya kuchukua hatua kukomesha jambo
hili tunakwenda mbele, tunakwenda nyuma…mbele, nyuma.
Hili haliwezi kuruhusiwa
kuendelea. Ni jambo la kutia simanzi sana,”
amesema Rais Kikwete na kuendelea:
“Mmeyasema
wenyewe…leo kiwanja hiki kinapitisha abiria milioni 2.5 kwa mwaka, mkifikisha
abiria milioni sita si mtakuwa soko huria kabisa…..mara leo mwanamuziki huyu
kakamatwa Afrika Kusini…mara kesho yule….limalizeni hili haraka.
Nataka
tuongeze usalama sana katika viwanja hivi viwili…. vimekuwa kama uchochoro.”
Rais
Kikwete amemtaka Waziri wa Uchukuzi kumjulisha ni maofisa gani wa Idara za
Serikali wanahusika kupitisha madawa hayo kwenye viwanja hivyo:
“Kama
kuna maofisa wa ushuru, ama maofisa wa uhamiaji, ama maofisa wa polisi ama
maofisa wa uwanja wa ndege ambao wanashiriki katika mchezo huu wa kupitisha
madawa haya nipeni orodha yao,
nitawaondoa kazini. Tusifanye masihara na hili, linatuaibisha sote.
Tusiwaonee aibu watu katika jambo hili.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
24 Aprili, 2014
Post a Comment