ASKARI wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto |
Baba Mzazi wa mtoto aliyeibiwa Salehe Issah Mwangosi(31) ndiye alieshirikiana na polisi huyo kumwiba mtoto |
Mboka Mwakikagile(20) mama mzazi wa mtoto aliyeibiwa |
ASKARI wa
Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP
5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa
mtoto jinsia ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe,
aliyeibwa April 6 mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela
Mkoani Mbeya.
Mtoto
alizaliwa Machi 30 na alipoibiwa alikuwa na umri wa siku sita ambapo
mtuhumiwa alishirikiana na Baba Mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe
Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama
mzazi aliyefahamika kwa jina la Mboka Mwakikagile(20) kuwa Prisca ni
shangazi yake Salehe hivyo anakuja kumwona mtoto aliyezaliwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kukamatwa kwa Askari
huyo ambapo amesema kuwa ikithibitika kutenda kosa hilo atafikishwa
mahakama ya kijeshi na baada ya taratibu hizo kukamilika atafikishwa
Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Mtuhumiwa
amekamatwa April 17 mwaka huu huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya
saa nne asubuhi akiwa na mtoto huyo mkononi ambapo alitiwa nguvuni na
kufikishwa makao makuu ya Polisi Mkoa Forest ya Zamani kwa mahojiano
zaidi.
Msangi
amesema kuwa Salehe na Prisca hawana mahusiano ya Damu ila wana
mahusiano ya kibiashara ambapo wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio
hilo na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazo wakabili.
Na Mbeya yetu
Post a Comment