Watu 21
wamefariki dunia katika ajali mbaya imetokea Wilaya ya
Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 3 na wengine 11
kujeruhiwa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema
ajali hiyo
imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri,
wilayani humo.
Awali ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hiace (T 948 CUX),
iliyokuwa ikitokea Ikwiriri kuelekea Rufiji ambalo lilikwenda
kukwaruzana na Lori(T 132 AFJ) kwa nyumba, ambalo lilikuwa limeharibika
na kusimama barbarani.
Alisema baada ya kulikwaruza roli hilo, mlango wa Hiace uling'oka na
kubaki kwenye roli ambapo gari hiyo lilipoteza mwelekeo na kwenda
kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Canter(T 774 CJW) na
kupinduka.
"Katika ajali hii, watu 14 walifariki dunia papo hapo, wakati polisi
na baadhi ya wananchi wakiendelea kuwaokoa majeruhi ili wakimbizwe
hospitali, likatokea basi la kampuni ya Mining (President)( T 242 BXA),
kuwakanyaga watu waliokuwa wakitoa msaada na kuwaua ndio maana idadi ya
waliokufa imefikia 21.
"Basi hili lilikuwa linatoka Lindi kuelekea Dar es Salaam...polisi
walifanya jitihada za kulisimamisha lakini dereva wake alikataa kusimama
na kwenda kukanyaga watu lakini tayari tumemkamata, majeruhi mmoja
amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam," alisema
Kamanda Matei.
Kamanda Matei alisema, basi hilo linashikiliwa polisi ambapo
uchunguzi ukikamilika, dereva wake atafikishwa mahakamani kujibu
mashtaka.
Aliwataja waliokufa ni Sixtus Ally Mtanga(32) na Nassoro Mohamed
Kajani(20) wakazi wa Ikwiriri, Juma Said Kitambulilo(30) na Salum Goma
Makonde (50), Ustaadhi Kalilambwe(34) na Shafil Kip (30), Wasabi
Sabil(45), Ramadhani Ally (23)wote wakazi wa Mbagala.
Shabani Bakari(30) Kondakta wa Hiace, mkazi wa Kibiti, Masud Abulal
(27), mkazi wa Mkuranga, Ammi Mpemba (30)na Madadi Hassan Mangasongo
(45) wakazi wa Jaribu na Japhet Ponsian (24), mkazi wa Dar es Salaam.
Pia yupo Said Ally China (21) mkazi wa Kimanzichana, mkazi wa Jaribu,
Abdalahaman Yusuph Kihemke(45), mkazi wa Kongowe na Fikiri Said Sauze,
mkazi wa Vikindu.
Wengine ni Nywari Mshigani mkazi wa Dar es Salaam, Hassan Wasabi
(18), mkazi wa Kibiti na Seleman Mcharazi (47) mwingine aliyejulikana
kwa jina moja la Mustafa, wote wakazi wa Mbagala na maiti ya mwanamke
haijafahamika jina lake.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Frank Sixmundi (31), dereva wa
gari la Maliasili Kibiti ambaye alifika eneo ili kutoa msaada kwa
majeruhi ambaye ameumia kichwani, Mohamed Salehe (49) na Charles
Rogasani (23), wote wakazi wa Kibiti na Mohamed Mengine (42), mkazi wa
Dar es Salaam.
Wengine ni Mniko Magige Mango (54) na Abdalah Issa
(25) wakazi wa Mkuranga, Khalid Salum (32), mkazi wa Dar es Salaam,
Ahmad Yusuph (23), mkazi wa Kigamboni na Shomari Yusuph (42), mkazi wa
Mburahati. Majeruhi wamelazwa katika hospitali za Ikwiriri, Misheni ya
Mchukwi na wengine hospitali ya Taifa Muhimbili.
Post a Comment