![]() |
| MADAKTARI wa Hospitali ya Holy Family (HFH)wanapigania maisha ya mtoto aliyezaliwa Septemba 25, mwaka huu akiwa na sura mbili na uzito wa kilo 3.2. |
Kwa
mujibu wa taarifa za hospitalini hapo, mtoto huyo mara baada ya
kuzaliwa amekutwa ana tatizo la kupumua hivyo kumlisha kupitia mdomo,
mpashaji aliliambia Gazeti la The Express Tribune.
Mtoto
huyo ni wa tatu kuzaliwa kutoka kwa Bi. Shahida Perveen na mumewe
Khalil Ahmed. Msajili wa hospitali hiyo, Dk. Qaisar Aziz ameliambia The
Express Tribune kwamba mtoto huyo amehamishiwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit) katika wodi ya watoto na atakuwa
katika uangalizi wao.
Hata
hivyo, madaktari wameonesha kukata tamaa na kusema kuna uwezekano mdogo
kwa mtoto huyo kuendelea kuishi na kukua. “Kumlisha kwa kutumia mdomo
haiwezekani kwa sasa, tunamlisha kwa kutumia mipira maalum (Naso-gastric
tube). Sura hizi mbili zinafanana,” alisema Dk Qaisar.
Habari
zinasema mama wa mtoto huyo alipopimwa na mashine maalum, (Ultrasound)
alionekana hana matatizo yoyote na alikuwa na afya njema.
Baadhi ya
wananchi waliotoa maoni yao kufuatia tukio hilo, walisema dunia
imetikisika kufuatia kuzaliwa kwa mtoto huyo wa ajabu na kuongeza kuwa
hiyo ni ishara kwamba imefika mwisho.

Post a Comment