
Ligi daraja ya tatu ngazi ya mkoa yameanza leo wilayani Liwale mkoani Lindi,pia mbunge viti maalum mh.Latifa kigwalilo aliuzulia uwanjani na alitoa jezi na mipira kwa timu zinazoshiriki ligi
Mechi ya ufunguzi ilikuwa Vijana star Vs kijiwe fc mchezo uliochezwa katika uwanja wa wilaya ya liwale.
Katika kipindi cha kwanza timu zote hakubahatika kuona lango la mwezake
Katika kipindi cha pili timu ya Vijana star ilijipatia goli 1 lilofungwa na
Ramadhani hashimu mpaka dakika 90,zinamalizika matokeo yalikuwa Vijana star 1-0 kijiwe fc
Kesho kutakuwa na mchezo kati ya mikukuyumbu world soccer Vs stand worriers timu ya kutoka lindi
"Chama cha mpira wa miguu liwale kinatoa shukrani za dhati kwa Wa viti maalum mh. Mbunge mama kigwalilo kwa msaada wake wa jezi na mipira kwa timu zetu zote za wilaya ya liwale zinazoshiriki ligi hii. Vifaa hivyo alivikabidhi mwenyewe uwanjani". alisema Ajali Kimbwembwe Katibu mkuu LIDIFA
Post a Comment