0
Arsene Wenger na Alexis Sanchez
Image captionArsene Wenger na Alexis Sanchez
Manchester United imewasilisha ombi la dau la £25m kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na raia wa Chile Alexis Sanchez. (Guardian)
Sanchez angependelea kujiunga na Manchester City, lakini kikosi cha Pep Guardiola kinataka kumsajili mchezaji huyo kwa £20m pekee. (Independent)
Manchester United pia wanawataka washambuliji wawili akiwemo mshambuiaji wa Leicester na Uingereza ,30, Jamie Vardy na mwenzake wa West Ham, 29, Javier Hernandez, ambaye alikuwa katika uwanja wa Old Trafford kutoka 2010-2015. (Telegraph)
Mshambuliaji wa West Ham Javier Hernandez
Image captionMshambuliaji wa West Ham Javier Hernandez
Klabu ya ligi ya New MLS nchini Marekani Los Angeles FC pia inamtaka Hernandez. (Talksport)
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte huenda akaondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri na aliyekuwa kocha wa Barcelona Luis Enrique wanaongoza kurithi mahala pake. (Mail)
Kocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique
Image captionKocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique
Manchester United na Chelsea wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 21, kutoka Gremio. (Star)
Liverpool wameanza mazungumzo na Leicester na winga wa Algeria Riyad Mahrez, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anataka kujiunga na Arsenal (Express)
Mshambuliaji wa RB Leipzig Naby Keita
Image captionMshambuliaji wa RB Leipzig Naby Keita
Liverpool inawasiliana na klabu ya RB Leipzig huku wakijaribu kumchukua mshambuliaji Naby Keïta kama mrithi wa Philippe Coutinho's aliyehamia Barcelona.
Mpango tayari umeafikiwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kujiunga na klabu hiyo mwezi Julai.(Times)
Liverpool iko tayari kumuuza mshambuliaji wao mwenye umri wa miaka 28 Daniel Sturridge, lakini watahitaji £30m ili kumuuza mshambuliaji huyo wa Uingereza. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Liverpool na Uingereza Daniel Sturridge
Image captionMshambuliaji wa Liverpool na Uingereza Daniel Sturridge
Hatahivyo hakuna klabu katika ligi ya Uingereza ilio na uwezo wa kumunua mchezaji huyo mbali na mshahara wake wa £150,000 kwa wiki . (Mail)
Raia wa Itali Carlo Ancelotti ndiye kocha anayepigiwa upato kumrithi mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu .
Kocha huyo wa zamani aliyewahi kuifunza Chelsea, Real madrid, Bayern Munich na Paris St Germain amekubali mkataba wa miaka minne wenye thamani ya £35.5m. (Corriere dello Sport - in
Carlo Ancelotti ndiye kocha anayepigiwa upato kumrithi mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu .
Image captionCarlo Ancelotti ndiye kocha anayepigiwa upato kumrithi mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu .
Everton inajiandaa kuwasilisha ombi la £20m ili kumsajili winga na mshambulijia wa Arsenal Theo Walcott. (Telegraph)
Crystal Palace wanawalenga washambuliaji wawili. Wamekubaliana kulipa dau la £12m kumsajili mshambuliaji wa Senegal mwenye umri wa miaka 28 Diafra Sakho na itawasilisha ombi la dau la £13m kumsajili mshambuliaji wa Everton ,27, Oumar Niasse. (Evening Standard)
Claude Puel amethibitisha kwamba mshambuliaji wa Nigeria na Leicester Kelechi Iheanacho hataondoka Leicester City katika dirisha la uhamisho la mwezi huu
Mshambuliaji wa Nigeria na Leicester Kelechi Iheanacho
Image captionMshambuliaji wa Nigeria na Leicester Kelechi Iheanacho
Mkufunzi wa The Foxes amemtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kuimarika katika kwa jumla. (Leicester Mercury)
West Ham wamepata pigo kutoka kwa mkufunzi wa Swansea Carlos Carvalhal ambaye amesisitiza kumzuia beki Alfie Mawson, 23, akidai kwamba klabu hiyo huenda ikamuuza iwapo itapokea ombi lisilopungua dau la £50m. (Star)
Christian Pulisic
Image captionChristian Pulisic
Manchester United itashindana na Liverpool katika kumwania mchezaji wa Borussia Dortmund na Marekani Christian Pulisic iwapo wapinzani wao watawasilisha ombi la kutaka kumsajili mchezaji huyo ,19, (Independent)
Manchester United inajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk's na Brazil Fred, 24, ambaye pia anasakwa na Manchester City(Record).
Espanyol wamepata habari kuhusu hamu ya klabu ya Stoke City kumchukua mkufunzi wake raia wa Uhispania Quique Sanchez Flores. (Marca - in Spanish)

Post a Comment

 
Top