BAADA
ya mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai kupiga marufuku
mifugo kulishwa na kunyweshwa katika vijiji ambavyo havijawapokea
wafugaji. Baadhi ya wafugaji waliangusha vilio mbele ya mkuu huyo wa
wilaya huku wakimuomba awahurumie ili mifugo yao isife kwa kukosa maji.
Hayo
yalitokea Octoba 3 katika kijiji cha Somanga Kusini wakati wa kikao cha
wafugaji na mkuu huyo wawilaya ambae alikwenda kukutananao ili
kusisitiza agizo lake la kuwataka wakulima waliovamia maeneo
yaliyotengwa kwa ufugaji wahame, na wafugaji waache kwenda kulisha
kwenye maeneo na vijiji ambavyo sio miongoni mwa vijiji 22 vilivyokubali
kuwapokea na kuishi nao.
Wafugaji
hao walisema agizo hilo litasababisha mifugo yao kufa kwakosa maji.
Kwasababu lambo walilokuwa wanatumia kunyweshea limekauka. Hivyo
wanalazimika kwenda kunywesha vijiji ambavyo sio miongoni mwa
vijiji vilivyoridhia kuwapokea.
Ikiwamo kijiji cha Kinjumbi ambacho wananchi wake wanalalamika kuvamiwa na makundi ya ng'ombe nakuharibu mazao ya kilimo.
Wafugaji
hao licha ya kutakakujua watanywesha wapi mifugaji yao badala ya
Kinjumbi, walisema sababu ya kukauka lambo walilokuwa wanatumia ni
wakulima kuvamia na kuendesha shuguli za kilimo kwenye maeneo
yaliyotengwa kwa ufagaji.
Mzee
Kazamoyo Makwaya, huku akidondosha machozi alisema serikali imeamua
kuwafilisi ili wawe masikini. Kwamadai kwamba mambo mengi waliyohaidiwa
na serikali wakati wanahama kutoka Ihefu kuja mikoa ya kusini kwakiasi
kikubwa hayatekelezwa.
"Tuliahadiwa
majosho, shule, marambo, madawa na maeneo ya kufugia, lakini tangu
nimekuja ninamiaka tisa hakuna yaliyofanyika zaidi ya lambo ambalo
linamefukiwa na wakulima," alisema mzee Kazamoyo.
Mzee huyo(70) alisema hawapeleki mifugo katika vijiji hivyo kwa kiburi lakini hawana njia ya kuokoa mifugo yao kufa.
Nganga
Mbeho, alisema wanaishi na kunyanyaswa kama sio raia halali. Kwamadai
kuwa eneo lilotengwa limevamiwa nawakulima, mifugo hata inapokula mabua
makavu ya mazao yaliyovunwa wanaadhibiwa.
Alisema mwaka huu pekee wamelazimika kulipa takribani 27.00 milioni kama faini. Huku kesi nyingi zinaendelea mahakamani.
Mfugaji
mwingine, Donalt Mbaga, alisema sababu ya migogoro baina yao nawakulima
nikutoheshimiwa mipaka na maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya matumizi
mbalimbali.
Mfugaji
huyo alisema iwapo wataheshimu mipaka na maeneo hayo itakwisha
tupotayari kushirikiana na serikali, hata lile lambo tupotayari kufukua
ikiwa serikali itatia nguvu pia.
Lakini kwa sasa mifugo tutanywesha wapi, maana tukiheshimu agizo tunahalalisha mifugo yetu ife kwa kiu," alisema Mbaga huku akimwaga machozi.
Akijibu hoja, malalamiko na maombi ya wafugaji hao, Ngubiagai alisema chanzo cha migogoro mingi ni baadhi ya viongozi, watendaji na wananchi kushindwa kutii, kusimamia na wengine wanapindisha sheria kwa masilahi yao binafsi.
Hivyo yeye hapendi na hatarajii kuwa nimiongoni mwa wasiotii sheria na wanaosababisha migogoro badala ya kutatua.
Aliwataka
wafugaji hao kushirikiana na serikali katika kushugulikia changamoto
walizonazo kwenye eneo walilopewa, badala yakupeleka mifugo maeneo na
vijiji yasivyo husika.
"Ofisa
mifugo tafadhali waoneshe haraka maeneo yanayopatikana maji katika
vijiji 22 vilivyokubali kuwapokea waende wakati tushugulikia changamoto
hizo," alisema Ngubiagai.
Mkuu
wa wilaya alisisitiza wakulima waliovamia maeneo yaufugaji waondoke
ndani ya wiki mbili. Nawafugaji waache kupeleka mifugo katika maeneo
yasiyositahili.
Wilaya
Kilwa hadi sasa ina upungufu wa ngombe 56437 wanaoweza kujaza maeneo
yaliyotengwa kwa ufugaji. Kwasababu hadi sasa inadadi ya ng'ombe 27279
tu, wakati mahitaji halisi ni ng'ombe 83427.
Post a Comment