Wandishi wa habari wakifuatilia tarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa na mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed
alipokuwa akijibu maswali ya wandishi wa habari katika Mkutano wake
Ofisini kwake Vuga.
Waziri wan chi ofisi ya makamo wa pili ya rais Mohammed Aboud Mohammed amesema uchumi wa Zanzibar unazidi kuimarika kwa karibu ya asilimia saba na mfumuko wa bei bado upo kwenye tarakimu moja na pato la Taifa linazidi kukua.
Ametoa maelezo hayo ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi Serikali ya awamu ya saba kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein.
Amesema katika awamu hii kwa ujumla harakati za uchumi zinaendelea vizuri na ishara zote za kuimarisha uchumi katika mwaka huu wa fedha zinatoa sura nzuri za mafanikio.
Akizungumzia suala la Muungano amesema unaendelea kuimarika na vikao mbali mbali vya watendaji wakuu wa pande mbili wakiwemo mawaziri vimeshafanyika na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ameshafanya vikao viwili vya kisekta kwa nia ya kutatua changamoto zilizopo.
Waziri Aboud ameelezea kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekamilisha kazi ya kuipandisha hadhi iliyokuwa Idara ya upigaji chapa na mpigaji chapa mkuu wa serikali na kuwa wakala wa serikali wa uchapaji.
Aidha amesema kazi ya kufunga mitambo mipya ya uchapaji imekamilika na mafundi wa kiwanda hicho wanaendelea kupatiwa mafunzo ili kuimudu teknolojia mpya ya mitambo hiyo ili kuongeza ufanisi na kuongeza upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati.
Sambamba na hayo Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kupitia Tume ya kitaifa ya kuratibu na udhibiti madawa ya kulevya imepania kutoa athari za madawa ya kulevya kwa jamii.

Post a Comment