![]() | |
|
SPIKA wa
Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko ya wajumbe wote 24 wa Kamati ya
Bunge ya Masuala ya Ukimwi kwa kuunda upya kamati hiyo na kuteua wajumbe
wapya 16, ambao pia watakuwa ni wajumbe katika kamati nyingine za
Kudumu za Bunge.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge
jana kwa vyombo vya habari, mabadiliko hayo yamelenga kuwawezesha
wabunge kujifunza na kujipatia uelewa na uzoefu zaidi katika kutekeleza
shughuli mbalimbali za Kamati za Bunge, ambapo wabunge wote waliokuwa
wajumbe wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi awali, wamepangiwa Kamati zingine
kwa nia ya kuboresha Utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
“Msingi
wa mabadiliko haya unatokana na Ibara ya 96 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inayolipa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mamlaka ya kuunda Kamati za Bunge za namna
mbalimbali kadri linavyoona inafaa, kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji
wa majukumu yake na Kanuni ya 116 (3) – (5) ya Kanuni za Kudumu za
Bunge Toleo la Januari, 2016 inampa Spika mamlaka ya kuteua wabunge ili
wawe wajumbe katika Kamati mbalimbali za Bunge, ikiwa ni pamoja na
mamlaka ya kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza idadi ya wajumbe
katika Kamati za Kudumu za Bunge,” ilieleza taarifa ya Bunge.
Ilieleza
kuwa kwa mujibu wa Waraka Na.5/2016 wa Spika kwa wabunge wote wa Oktoba
7, mwaka huu, mabadiliko haya yataanza kutekelezwa mara moja kuanzia
mwezi huu ambao wajumbe husika watakutana kwa ajili ya kufanya uchaguzi
wa viongozi wao na kuandaa ajenda za vikao vya kamati.
Taarifa
hiyo iliwataja wajumbe wapya 16 wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi
na kamati zao nyingine katika mabano kuwa ni Asha Abdullah Juma (Katiba
na Sheria), Daniel Mtuka (Sheria Ndogo), Dk Faustine Ndugulile (Huduma
na Maendeleo ya Jamii), Dk Hadji Mponda (Mjumbe wa PAC), Dk Jasmine
Bunga (Huduma na Maendeleo ya Jamii), Gibson Meiseyeki (Katiba na
Sheria), Joseph Mhagama (Katiba na Sheria), Juliana Shonza (Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama).
Wengine
ni Kemirembe Lwota (Ardhi, Maliasili na Utalii), Lucia Mlowe (Huduma na
Maendeleo ya Jamii), Mary Muro (Miundombinu), Martha Mlata (Viwanda,
Biashara na Mazingira), Masoud Abdalla Salim (Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama), Oscar Mukasa (Nishati na Madini), Stanslaus Nyongo (Viwanda,
Biashara na Mazingira) na Yussuf Kaiza Makame (Nishati na Madini).
Waliohamishwa
na kamati katika mabano ni Hassna Mwilima (Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama), Constantine Kanyasu (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC),
Muhammed Amour Muhammed (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Sixtus
Mapunda (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Juma Kombo Hamad (Katiba na
Sheria), Mattar Ali Salum (Kilimo, Mifugo na Maji), Savelina Mwijage
(Huduma na Maendeleo ya Jamii), Khalifa Mohammed Issa (Utawala na
Serikali za Mitaa), Abdallah Haji Ali (Hesabu za Serikali (PAC), Waitara
Mwikabe (Utawala na Seikali za Mitaa), Khamis Yahya Machano (Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama) na Sikudhani Chikambo (Huduma na Maendeleo ya
Jamii).
Wengine
ni Zuberi Kuchauka (Miundombinu), Mgeni Jadi Kadika (Hesabu za Serikali
za Mitaa (LAAC), Hussein Amar (Huduma na Maendeleo ya Jamii), Richard
Mbogo (Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Grace Tendega (Huduma na
Maendeleo ya Jamii), Elibariki Kingu (Sheria Ndogo), John Kadutu (Hesabu
za Serikali za Mitaa (LAAC), Azza Hillal (Hesabu za Serikali za Mitaa
(LAAC), Zaynab Vulu (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), John Heche
(Nishati na Madini), Vuma Augustine (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)
na Yahya Masare (Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama).

Post a Comment