Mapumziko ya siku moja, kikosi cha Mbeya City FC leo Octoba 9 kimeanza rasmi mazoezi kujiweka sawa tayari kwa mchezo mwingine wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba SC uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jumatano ijayo hii ikiwani siku tano tu baada ya suluhu ya bila kufungana na Stand United.
Ofisa
Habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema kwamba nyota kadhaa waliokosa
michezo miwili iliyopita kutokana na majeraha wamekuwa sehemu ya kikosi
kilichofanya mazoezi asubuhi ya leo tayari kwa kuivaa Simba Sc siku
ya jumatano.
Alisema
kwamba kikosi chake kilicheza vizuri mchezo uliopita dhidi ya Stand
United na kufanikiwa kutawala mchezo wa dakika zote, lakini safu ya
ushambuliaji haikuwa na bahati licha ya kujaribu mara kadhaa kupiga
mashuti yaligonga mwamba.
“Tulikuwa
na mchezo mzuri dhidi ya Stand, kwenye soka wakati mwingine bahati huwa
ina nafasi yake, Simba wajiandae vya kutoasha kwa sababu tumedhamiria
kufunga magoli mengi,tunajua tabia zao wanapofungwa lakini uwanja wa
Sokoine una sura nyingine, jambo muhimu kwa waamuzi tunaomba wachezeshe
mchezo kwa kufuata sheria 17, ili mashabiki wapate burudani na
kufurahia ushindi kwa timu yao”, alimaliza.
Post a Comment