Kuna wakati huwa tunajisikia vibaya na kujihisi kama kukata tamaa,
kutokana na hali ya kushindwa kutimiza malengo yetu kwa muda muafaka
tuliojiwekea.
Najua ni kitu ambacho wakati huwa kinauma hasa pale unapoona malengo yako hayatimii upesi kama unavyotaka iwe. Je, ni kitu gani unachotakiwa kufanya hasa unaona malengo yako hayajatimia kwa muda muafaka?
1. Weka mipango yako upya.
Kama mbinu ambazo umezitumia kufanikisha malengo yako hazijakusaidia kufikia malengo yako kwa wakati, panga malengo yako tena upya. Acha kujiona umepoteza sana, weka malengo yako upya na jaribu tena na tena na tena.
2. Kuwa king’ang’anizi.
Pale malengo yako yanaposhindwa kutimia kwa wakati jaribu kuwa king’ang’azi. Usije ukaingia katika hali ya kukakata tamaa, kwa sababu hali ya kukata tamaa haiwezi kukusaidia sana zaidi ya kukukwamisha tena.
3. Hamasika na mafanikio ya wengine.
Hata kama mambo yako yamekuwa magumu na malengo yako yameshindwa kutimia kwa wakati, ili kurudi kwenye mstari jaribu kutumia njia ya kuhamasika kwa kuangalia mafanikio ya watu wengine.
4. Angalia changamoto zilizokuzuia.
Pia ni kweli umeshindwa kufika pale ulipotaka kufika kwa wakati, sasa ni vyema ukaangalia changamoto zile zilizokuzuia kufanikiwa. Ukishazitambua changamoto hizo zinafanyie kazi mara moja na kisha songa mbele.

Post a Comment