Akitao tamko juu ya siku ya maadhimisho ya kupinga adhabu ya kifo
duniani ,mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Dk Hellen Kijo Bisimba
amesema adhabu ya kifo imekuwa kinyume na siyo sahihi.
“Adhabu hii inakuwa kama ya kulipiza kisasi,kwasababu haimsaidii yule
aliyekufa zaidi ya kuongeza mtu mwingine kufa, hata ndugu wanaosema
ndugu yetu amekufa akiuawa huyo aliyeuwa wao hawampati tena ndugu yao
kwahiyo haisaidii,” alisema.
“Lakini pia utafiti haujaweza kutuonyesha kwamba adhabu hii imesaidia kuondoa hilo tatizo,” aliongeza Bisimba.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikishinikizwa na
mashirika ya kimataifa hasa yale ya utetezi wa haki za binadamu kufuta
sheria hiyo.
Machi 6 mwaka huu Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa,
Navi Pillay alinukuliwa kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la
Utangazaji la Uingereza (BBC) akilaani kuendelea kwa adhabu hiyo
alioyoiita kuwa ni ‘ukatili dhidi ya binadamu.’
Zaidi ya watu 360 wanasubiri adhabu hiyo nchini.
Post a Comment