Tangazo hilo limetolewa baada ya miezi
kadha ya maandamano dhidi ya serikali, yaliyofanywa na makabila mawili
makubwa ya Ethiopia ya Oromo na Amhara.
Makabila hayo yanalalamika kuwa yametengwa kiuchumi na kisiasa.
Ghasia baina ya waandamanaji na polisi zilizidi tangu watu 55 walipokufa
katika sherehe za kitamaduni za Oromo, Jumapili iliyopita.
Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema, mamia ya watu wameuawa, na maelfu kukamatwa tangu maandamano yalipoanza
Post a Comment