Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kulia), akizungumza na wajumbe wa
baraza la ardhi wa wilaya hiyo Dar es Salaam juzi, wakati wakipeana
mikakati ya kazi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya migogoro ya
ardhi.
Mkutano ukiendelea.
DC
Sophia Mjema (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa
mstaafu wa Dar es Salaam, mama Mary Chipungahelo (kulia) na Katibu
Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo.
DC Mjema akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza hilo.
Dotto Mwaibale
WAJUMBE
wa Baraza la Ardhi wa Wilaya ya Kinondoni wametakiwa kutobweteka badala
yake waende kwa wananchi ili kujua changamoto za ardhi katika wilaya
hiyo.
Mwito
huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Sophia Mjema Dar es Salaam
juzi alipokuwa akizungumza na wajumbe hao ofisini kwake.
"Ninyi
ni watu muhimu sana katika kuibua changamoto za ardhi katika kata zetu
zote za wilaya ya Kinondoni nawaomba msiwe watu wa kukaa nendeni kwa
wananchi huko kuna changamoto nyingi za ardhi" alisema Mjema.
Mjema
aliwataka wajumbe hao kwenda kutoa elimu kwa wananchi ili wajue haki
zao kuhusu masuala ya ardhi jambo litakalosaidia kupunguza migogoro ya
ardhi.
Aliongeza
kuwa migogoro mingi ya ardhi iliyopo katika wilaya hiyo mingi
inasabaishwa na wananchi kutojua masuala ya ardhi na elimu.
Post a Comment