Mkazi wa mtaa wa Omukishenye ulioko katika kata ya Hamgembe
iliyoko katika manispaa ya Bukoba, John Nkyoiga aliyelazimika kuishi
kwenye nyumba yake iliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea
mkoani Kagera kwa kukosa Maturubai yaliyokuwa yakisambazwa na serikali
amenusurika kifo baada ya kuangukiwa na ukuta zake nyumba hiyo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo wakati wa mvua iliyonyesha huku ikiwa na upepo mkali, akizungumza na ITV Nkyoiga amesema baada ya kuangukiwa na ukuta ameopolewa na majirani baada ya mke wake Maida Said kupiga kelele za kuomba msaada, amesema tangu tetemeko litokee septemba 10, mwezi uliopita hajawahi kupata msaada wowote wa kibinadamu na ndio maana analazimika kuishi kwenye nyumba yake yenye iliyobomoka.
Nao baadhi ya wananchi katika kata ya Hamgembe ambao hawajapokea msaada wowote wa kibinadamu tangu litokee tetemeko la ardhi leo wamewapa wakati mgumu waandishi wa habari waliofika kwenye eneo la Omukishenye kwa kuwafukuza katika eneo hilo wakidhani ni maofisa wa serikali wanaoambaza misaada ya kibinadamu ambao hawajawafikia , wakizungumza kwa jazba na waandishi hao wamesema kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu.
Source: Itv

Post a Comment