0


 Maendeleo endelevu inahitaji amani endelevu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika hotuba yake katika mkutano na viongozi wa kundi la nchi 20, G20 unaoendelea Hangzhou, China.

Katika mkutano huo wa kila mwaka, viongozi wa mataifa hayo yaliyoendelea kiuchumi Zaidi duniani wanajidili masuala ya kiuchumi , ambapo Katibu Mkuu Ban ametoa msisitizo kwa nchi hizo kutoa jitihada zaidi katika ajenda ya maendeleo endelevu,SDGs, ambayo nchi wanachama walitia saini mwaka jana.

Ban amesema maendeleo hayoyanawezekana tu katika nyakati za amani…
Maendeleo endelevu yanahitaji amani endelevu. Ili ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu kufanikiwa, ili ukuaji wa uchumi imara kuwa na mafanikio, tunahitaji amani na maendeleo kwenda mkono kwa mkono. Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia mataifa mpito, katika jitihada zao za kuhakikisha upatikanaji wa amani, maendeleo na haki za binadamu.  “

Post a Comment

 
Top