0

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa tamko
la kubadilishwa kwa sera za nchi yake katika
masuala ya kubadilishana ama kuwakomboa
mateka ambao ni raia wake.
Rais ametiulia mkazo kauli yake, amesema
kwamba seriakali yake haitafanya
makubaliano yoyote yenye lengo la
kuwakomboa mateka ambao ni raia wa
Marekani waliotekwa ughaibuni,lakini aliweka
bayana juu ya familia ambazo huamua kulipa
fidia ya ndugu zao mateka kwamba
hawatakabiliwa na mashtaka.
Rais Obama ameeleza kuwa anatambua wazi
kuwa familia za mateka huwa
wanachaganyikiwa pindi wanapo shughulika
na serikali yao wenyewe.
Ameelezea pia mipango ya baadaye ya
serikali yake na sera za nchi hiyo kwamba
kutakuwa na utaratibu maalum kiserikali
kuratibu jitihada za vitengo mbali mbali na
taasisi zingine zinazojitahidi kuwaokoa
mateka ambao ni raia wa Marekani .Ahadi ya
Rais Obama kwa raia wake ni kuchukua hatua
stahiki kuwarejesha raia wake nyumbani na
kuwachukulia hatua watekaji wao.
Ujumbe wangu kwa kila raia wa Marekani
ambaye anashikiliwa mateka popote
ulimwenguni,ni huu Marekani haitaacha
kuhakikisha unaungana na familia
yako.hatutasita,hata kama itatuchukua muda
mrefu kiasi gani.

Rais wa marekani Barak Obama

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top