0

Timu ya mitumba fc livalia jezi rangi nyeupe na timu ya Super stars ilivyalia jezi nyeusi na njano

Timu ya Mitumba fc imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Super stars fc hatua ya robo fainali ligi ya Alizeti cup mchezo uliopigwa katika uwanja wa wialaya ya Liwale mkoani Lindi.

katika mchezo huo katika kipindi cha kwanza timu zote zilipumzika zikiwa sare bila kufungana hata kipindi cha pili hakuna timu iliyoweza kutikisa nyavu za mwezake.

Baada ya dakika 90 kukamilika kwa mujibu wa kanuni za ligi hii kutakuwa na hatua ya matuta ndipo ilipopigwa mikwaju ya penaiti.

Timu ya Mitumba fc ilikuwa ya kwanza kupiga penaiti lakini iliweza kupoteza mkwaju wa kwanza na wa pili huku super stars ikipata penaiti 2 za mwanzo na kila golikipa aliweza kukamata penaiti moja moja baada ya kupiga penaiti 5 na kutoka sare ya goli 2-2 ikaongezwa penaiti moja moja katika nafasi hiyo super stars ilitumia vema nafasi hiyo huku Mitumba fc iliweza kupoteza na matokeo yakawa Super stars 3-2 mitumba fc








Post a Comment

 
Top