0

Tokeo la picha la INTERVIEW
Karibu penda msomaji wa blog yetu pendwa ni matumaini yangu bado unaendelea na harakati za kujenga taifa bila kukata tamaa sambamba na juhudi katika kufanikisha malengo yako,ipo siku mambo yatakuwa muhimu ni subira na  kumbuka kwenye nia kuna njia siku zote.Uchumi wa nchi yetu siyo haba unakuwa ila tatizo la ajira sasa ni kama wimbo wa taifa hasa kwa vijana ambao ni nguvu ya taifa la kesho ila usithubutu kukata tamaa hata kidogo ukiamini jambo unalolifanya ipo siku litakuwa kwani Mungu hamnyimi mja wake.Leo katika blog yetu hii pendwa nitazungumzia kivipi inaweza kushnda usaili wa kazi kwa hatua ambazo ukizifanyia kwa uwezo wa mungu huwezi kukosa kazi.

      Kusanya taarifa za kutosha  hakikisha unakusanya  tarifa muhimu kuhusu kampuni au taasisi unayoenda kufanya usaili wako kama inahusika na nini,ilianzishwa mwaka gani n.k hizi zitakusaidia hasa kwenye kujibu maswali wakati wa usaili.

        Mavazi msailiwa ana budi kabla ya kuingia kwenye usaili afanye utafiti  wa mavazi ni aina gani ya mavazi yanapendelewa kuvaliwa na wafanyakazi wa hapo, kama ni suti hata kama ni jua kali basi huna budi kuvaa kama  huna jaribu hata kuazima.

        Heshima,tabasamu na bashasha heshima ni kitu muhimu sana kwa msailiwa jaribu kutoa salamu kwa watu wpte utakaokutana nao maana huenda mmoja kati ya hao akawa msaili pia unapoingia sehemu ya usaili.lugha ya vitendo pia ni kitu muhimu ikiendana na tabasamu watu bwa ulaya wanaita  body language kumbuka kuwa makini pia wakati wa kujibu maswali maana hapa ndi kwenye maana ya usaili.

         Hitimisho baada ya kumalizika usaili basi msailiwa huna budi kuwashukuru wasaili wako kama kuna swali unaweza kuwauliza hii itakusaidia kuonekana kama unajiamini zaidi .Baada ya yote pia jaribu kuomba Mungu.

Post a Comment

 
Top