0
Screen Shot 2017-01-19 at 9.16.01 AM
    
Raisi mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili sola kabisa.Infantino anaonekana kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta vyake.Baada ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48 sasa Infantino amekuja na mpya.Kwa kumtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten amependekeza baadhi ya sheria mpya katika soka.

Kuondoa offside.
Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.Alisema “sipati picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi nyingi sana za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa wakuvutia sana kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo litawafurahisha mashabiko na washambuliaji.

Kubadili upigaji wa penati.Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati.Kwa sasa adhabu ya penati mchezaji anauweka mpira mita kadhaa karibu na goli ma kuupiga.Lakini Van Basten anaona penati ibadilishwe.Anataka mpiga penati auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio ngeni kwani mwaka 1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.

Kupunguza adhabu mipira ya kushika.Van Basten anaona kama adhabu ya kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo.Na analiona kama tukio dogo lisilohitaji kadi nyekundu na anazani inapaswa ipunguzwe adhabu hiyo.Kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa.Adhabu kam ile ya tukio la Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika mpira wakati ukiingia golini Van Basten anataka kadi iwe ya njano.

Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi.Kama katika Rugby ni kapteni tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji yeyote kuongea na mwamuzi.

Style ya faulu ya mchezo wa kikapu.Katika mchezo wa kikapu pale mchezaji anapocheza faulu tano anatakiwa atoke uwanjani.Na sasa Van Basten anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.

Kupunguza idadi ya mechi.Hii itafurahiwa sana na makocha wageni Uingereza.Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi ya mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.

Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani kuongeza idadi ya wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba na sasa FIFA inatarajia kuliangalia suala hili.

Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua kutokana na kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya upigaji penati vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha dakika 10 za mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema watahakikisha hakuna upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.

Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA.Na sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze kujadiliw

Post a Comment

 
Top