0
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wanaoishi wanaoishi katika magumu cha Eco Village mkoa wa Pwani baada ya kuwakibidhi zawadi mbalimbali.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem ametembelea Kijiji cha Eco-Village kilichopo Kisemvule Mkoa wa Pwani. Eco-village ni eneo la kulelea na kuhudumia mayatima ambapo ndani yake kunafanyika shughuli za kilimo,ufugaji wanyama hasa kuku na ng'ombe, na hutegemea umeme wa jua kama chanzo cha nishati.

Katika ziara hiyo Mhe. Jasem  alikabidhi msaada wa vyakula unga wa ngano,mchele,maharage,mafuta ya kula,majani ya chai na sukari kwa ajili ya watoto mayatima msaada ambao utatosheleza kwa kipindi cha miezi miwili.

Pembezoni mwa ziara Mhe. Balozi alipanda mti ikiwa ni ishara ya kuunga mkoni juhudi za Eco-village ambacho ni kituo kinachoendesha mambo yake kisasa. 
 Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem  akipanda mti katika kituo cha watotot wanaoishi wanaoishi katika magumu cha Eco Village mkoa wa Pwani  alipikwenda kutembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.

Post a Comment

 
Top