0

 Mchezaji wa timu ya Sido fc akipiga adhabu ndogo kuelekea lango la timu ya Wachukuzi fc mchezo uliochezwa julai 28 katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi



 Mlinda mlango wa timu ya Wachukuzi fc akiwa kwenye harakati ya kuokoa mpira 


Timu ya Wachukuzi fc kwenye mchezo wao dhidi ya Sido fc katika Ligi ya Kazumari Cup julai 27 uliwavutia watazamaji wengi wa soka baada ya timu hiyo kuikaba koo Sido fc na kumaliza mchezo huo kwa sare ya kufungana goli 1-1 mchezo ulichezwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Wachukuzi waliweza kuimalisha kuta za ulinzi upande wa makibi na kuweza kuimili vishindi hivyo mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza hawakuweza kurusu goli.

Goli la kwanza la Sido fc lilifungwa na Abuu Kazumari namo dakika ya 53 na goli la kusawazisha la Wachukuzi lilifungwa na Rashidi Ubavu katika dakika ya 59.

Dakika ya 85 mchezaji wa timu ya Sido fc,Salumini Mmuka alipewa kadi nyekundi baada ya kucheza refu na kupelekea timu hiyo kucheza punguvu hata hivyo timu ya Wachukuzi fc hawakuweza kutumia vema nafasi hiyo.

Post a Comment

 
Top