0
Mbunge  wa  Lindi  mjini  Hasani Kaunje Asaidia wagongwa  hospital  ya  sokoini  Vyandarua  200  na  shuka  200


Mbunge wa jimbo hilo, Hassan Kaunje  amechangia vyandarua 200 katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi  Sokoine  Ikiwa  moja  ya  kuondoa  kero  na  kuunga  mkono juhudi za wananchi kujiletea maendeleo
 Tukio  hilo limefanyika  kwenye  hafla ya kukabidhi vyandarua hivyo, iliyofanyika hospitalini hapo, mbunge huyo alisema anazitambua changangamoto wanazokabiliana nazo wananchi na kiu waliyonayo katika kujiletea maendeleo.

 Mbunge huyo ambae jana alichangia mifuko 70 ya saruji ambayo 40 itatumika kujengea uzio wa shule ya msingi Rahaleo, na 30 ujenzi wa ofisi ya kata ya Mwenge. Alibainisha kwamba badala ya fedha zilizotumika kununua vyandarua hivyo kumpa mtu mmojamoja au kundi fulani aliona apeleke katika hosipitali hiyo.

Kwasababu zita wanufaisha wapiga kura wake na wengine wa nje na jimbo hilo watafaidika pia“Badala ya fedha hizo kununulia futari na kufuturisha, nimeona ninunue vyandarua ili mmbu wasiwafuturu nyinyi,” alisema kwa utani Kaunje

lisema anazijua baadhi ya changamoto zilizopo katika hosipitali hiyo muhimu. Ikiwamo kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa. Akiweka wazi kwamba hali hiyo inachangiwa pia na wilaya ya Lindi kutokuwa na hosipitali yake.

“Kuhusu suala hilo nimemueleza waziri mwenye dhamana ya wizara ya afya, jamii, jinsia, watoto na wazee. Pia kunatatizo la choo, naahidi kujenga pindi mkitupatia eneo la ujenzi huo, lakini pia ninaahidi kuleta mashuka 200,” alisisitiza Kaunje.
Aidha mbunge huyo alizungumzia changamoto ya uhaba wa fedha za ukarabati wa miundo mbinu ya hospitali hiyo na wataalamu. kuhusu hayo alisema mkoa umetenga takribani shilingi 185.00 milioni ambapo pia mwezi Julai kunafedha zitaletwa, kwani tayari zimetengwa. Huku akiwatoa hofu kuhusu uhaba wa wauguzi na madaktari kwa kusema.

“Kuna mgao wa manesi na madaktari, kinachosubiriwa idhini (kibali) ya kuajiri, basi tatizo hilo litakwisha kwasababu tutakuwa na mgao na nitachangia ujenzi wa jengo la kupumzika ndugu na jamaa za wagonjwa,” aliongeza kusema.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa hosipitali hiyo, Dkt Emmanuel Shija licha ya kushukuru kupata msaada huo, alisema hosipatali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kuondolewa ili iweze kutoa huduma kwa ufanisi. Shija alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni upungufu wa wawatumishi wapatao 200. Ambapo mahitaji ya madaktari katika vitengo ni 6. Hata hivyo inadaktari mmoja tu. Ikiwa na upungufu wa wauguzi takribani 100. “Changamoto nyingine ni maji, choo na umeme. Tunaomba pia kupewa tanki la maji la akiba tunatanki moja, ambalo linaonekana lipo kwenye hifadhi ya barabara,” alisema Shija.

Vyandarua hivyo vilikabidhiwa kwa meya wa manispaa ya Lindi na diwani wa kata ya Rahaleo, Mohamed Lihumbo ambae alikabidhi kwa uongozi wa hosipitali hiyo



Post a Comment

 
Top